Google Family Link ni programu ya vidhibiti vya wazazi inayokusaidia kuimarisha usalama wa familia mtandaoni. Kila familia ina uhusiano wa kipekee na teknolojia, kwa hivyo, tulibuni zana ili uchague uwiano bora kwa familia na kuisaidia kuwa na hali bora inapotumia teknolojia dijitali. Unaweza kutumia programu kuangalia jinsi mtoto anavyotumia kifaa pamoja na mahali kilipo, kudhibiti mipangilio ya faragha na zaidi.
Ukitumia Family Link, unaweza:
Kuweka miongozo ya matumizi ya dijitali
• Kuweka vikomo vya muda wa kutumia kifaa — Weka muda wa kutumia kifaa unaomfaa mtoto. Family Link hukuwezesha kuweka vikomo vya kila siku vya muda pamoja na ratiba za wakati wa shule na wa kupumzika kwenye vifaa vya mtoto, ili umsaidie kutumia muda vizuri.
• Kudhibiti programu za mtoto — Rahisishia mtoto matumizi ya programu. Weka vikomo vya muda wa kutumia programu mahususi na muda usio na kikomo kwa programu za kielimu au zinazotumika sana. Pia, unaweza kuzuia programu.
Kudhibiti usalama, faragha na vichujio vya maudhui
• Kudhibiti anachoona mtandaoni— Weka vidhibiti vya wazazi kwenye huduma za Google kama vile Chrome, Google Play, YouTube na Tafuta. Family Link hukuruhusu kuzuia tovuti zisizofaa, kuhitaji idhini ya programu mpya, kudhibiti ruhusa za programu na tovuti na zaidi.
• Kuimarisha usalama wa akaunti — Family Link hukuwezesha kudhibiti mipangilio ya akaunti na data ya mtoto. Ukiwa mzazi, unaweza kusaidia kubadilisha nenosiri la mtoto ikiwa atalisahau, kubadilisha taarifa zake binafsi au hata kufuta akaunti yake ikihitajika.*
*Watoto wenye umri unaozidi umri unaoruhusiwa wanaweza kudhibiti akaunti zao.
Kuendelea kuwasiliana popote ulipo
• Kuangalia waliko — Ni muhimu kuweza kuwapata wanafamilia popote waliko. Ukitumia Family Link, unaweza kutambua mahali watoto waliko kwenye ramani moja, mradi wamebeba vifaa vyao.
• Kupata arifa — Family Link hukutumia arifa muhimu ikiwa ni pamoja na mtoto anapoondoka au kufika mahali fulani. Unaweza pia kupigia vifaa na kuangalia muda wa matumizi ya betri uliosalia kwenye kifaa.
Maelezo Muhimu
• Zana za Family Link hutofautiana kulingana na kifaa cha mtoto. Angalia orodha ya vifaa vinavyooana katika https://families.google/familylink/device-compatibility/
• Ingawa Family Link hukusaidia kudhibiti vipakuliwa na ununuzi wa mtoto kwenye Google Play, hatahitaji idhini yako kuweka masasisho ya programu (yakiwemo masasisho yanayopanua ruhusa), programu ulizoidhinisha hapo awali au zilizotumwa katika Maktaba ya Familia. Idhini za ununuzi zitatumika tu mtoto anapofanya ununuzi kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play na hazitatumika anapofanya ununuzi kupitia mifumo mbadala ya utozaji. Wazazi wanapaswa kukagua programu zilizowekwa na ruhusa za programu za watoto katika Family Link.
• Unapaswa kukagua kwa makini programu zilizo kwenye kifaa cha mtoto kinachosimamiwa na uzime ambazo hungependa atumie. Kumbuka, huenda usiweze kuzima baadhi ya programu zilizowekwa mapema k.m. Google Play, Google, n.k.
• Ili uone mahali kifaa cha kijana au mtoto kilipo, ni lazima kiwe kimewashwa, kimetumika hivi majuzi na kimeunganishwa kwenye intaneti kupitia data au wifi.
• Vidhibiti vya wazazi vya Family Link vinapatikana tu kwenye akaunti za Google zinazosimamiwa. Watoto wakitumia Akaunti za Google zinazosimamiwa, wanaweza kufikia bidhaa za Google kama vile Tafuta, Chrome na Gmail na wazazi wanaweza kuweka miongozo ya matumizi ya dijitali ili kuwasimamia.
• Ingawa Family Link hukupa zana za kudhibiti hali ya mtoto mtandaoni na kuimarisha usalama, haifanyi intaneti kuwa salama. Family Link haiwezi kubaini maudhui yanayopatikana kwenye intaneti, lakini inakupa zana za kufanya uamuzi kuhusu jinsi mtoto anavyotumia muda katika kifaa na kubaini njia bora ya kudumisha usalama mtandaoni inayofaa familia.
Ilisasishwa tarehe
30 Apr 2025